NAMNA YA KUSAFISHA NA KUTUNZA KUCHA ZAKO
Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambayo utavitumia unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu. Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inayochangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya. Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi. Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, unapaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi. Ni vyema kwa mtu anayejali afya ya kucha zake kuchukua muda mwingi kufuatilia kuc...