JINSI YA KUTUNZA NGOZI YAKO KWA KUTUMIA LIMAO
Katika makala hii utapata kujua sababu
mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika. Mbali na hali ya
hewa pia matumizi ya pombe, sigara , cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na
watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa
ijitengeneze yenyewe na si kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani.
Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa
siku ni njia nzuri kama unataka kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu
ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na
matunda kwa wingi hata kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa
akitegemea kuwa na ngozi nzuri jambo ambalo ni gumu. Mara kadhaa tumeshuhudia
watu wanaopaka cream kali wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili
ukionekana kuwa mkavu
Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili
na hata unapowauliza baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado
wana ngozi nzuri zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha
wanatengeneza ngozi zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na
kuwa na madoa kutokana na kutumia make up kwa muda mrefu na hata anapogundua kuwa ana tatizo la madoa
amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo
jambo ambali linazidisha madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa
usoni kwa kutumia limao kwa sababu ile Vitamin C iliyopo
katika limao husaidia sana katika kuondoa chunusi kwa haraka.
JINSI
YA KUTIBU NGOZI YAKO KWA KUTUMIA LIMAO
unachotakiwa
ni kutumia maji ya limao yaliyo fresh na usiyalaze maji hayo kwa matumizi ya
baadaye kisha paka sehemu zilizoathirika kila unapolala usiku. Njia hii
itasaidia kukausha ngozi yako kutokana na mafuta yanayosababisha uvimbe.
Asubuhi unachotakiwa ni kwenda kunawa na maji ya vuguvugu mara kwa mara, pia
ijulikane kuwa njia hii siyo nzuri kwa
wale wenye ngozi laini sana.
Nitajaribu kwa imani
ReplyDelete