Afya


Katika makala hii utapata kujua sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika. Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe, sigara , cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa ijitengeneze yenyewe na si kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani. Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi nzuri jambo ambalo ni gumu. Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa mkavu
Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na kutumia make up kwa muda mrefu  na hata anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni  kwa kutumia limao kwa sababu ile Vitamin C iliyopo katika limao husaidia sana katika kuondoa chunusi kwa haraka.

JINSI YA KUTIBU NGOZI YAKO KWA KUTUMIA LIMAO
unachotakiwa ni kutumia maji ya limao yaliyo fresh na usiyalaze maji hayo kwa matumizi ya baadaye kisha paka sehemu zilizoathirika kila unapolala usiku. Njia hii itasaidia kukausha ngozi yako kutokana na mafuta yanayosababisha uvimbe. Asubuhi unachotakiwa ni kwenda kunawa na maji ya vuguvugu mara kwa mara, pia ijulikane kuwa  njia hii siyo nzuri kwa wale wenye ngozi laini sana.





Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.

Mafuta katika mwili yanatengenezwa na ‘sebaceous glands’,kwa hiyo kuna baadhi ya watu wana sebaceous glands ambazo zinatengeneza mafuta kwa wingi sana na hivyo kufanya ngozi zao kung’aa kwa sababu ya hayo mafuta mengi.
Sebaceous gland zipo kwa wingi usoni(face) shingoni(neck), kifuani,kichwani na mgongoni, ndiyo maana hayo maeneo yanakuwa na mafuta kwa wingi.

Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:

• Kurithi
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya hewa ya joto.


Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta

Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.






               
MAGONJWA YANAYOTIBIKA KUPITIA KITUNGUU SAUMU
  1. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
  2. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
  3. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
  4. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
  5. Huondoa Gesi tumboni
  6. Hutibu msokoto wa tumbo
  7. Hutibu Typhoid
  8. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
  9. Hutibu mafua na malaria
  10. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
  11. Hutibu kipindupindu
  12. Hutibu upele
  13. Huvunjavunja mawe katika figo
  14. Hutibu mba kichwani
  15. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
  16. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
  17. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
  18. Hutibu maumivu ya kichwa
  19. Hutibu kizunguzungu
  20. Hutibu shinikizo la juu la damu
  21. Huzuia saratani/kansa
  22. Hutibu maumivu ya jongo/gout
  23. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
  24. Huongeza hamu ya kula
  25. Huzuia damu kuganda
  26. Husaidia kutibu kisukari
  27. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
  28. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu

FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.







MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka:                                                                                                                                  
kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.



Comments

Popular Posts